.
Mkuu wa Jeshi la polisi Tanzania Simon Sirro amesema maagizo aliyotoa waziri wa Afya Dkt,Doroth Gwajima kuhusu Polisi na Takukuru kumkamata Mbunge wa Kawe Josephat Gwajima ameyasikia hivyo polisi wanasubiri maelezo ya maandishi
''Tumeyasikia hayo maelekezo,jambo la msingi unajua maelekezo ya kiserikali mara nyingi yanakwenda kwa maandishi,tunasubiri maandishi ya kuonyesha kuna kosa gani,maanake sisi tunashughulika na makosa ya jinai ,kwahiyo nasubiri maelekezo kutoka kwake halafu tutaangalia kama ni makosa ya jinai tutachukua hatua na kama tutaona ni vinginevyo tutashauri njia nyingine itumike badala ya kutumia Jeshi la polisi''. IGP Simon Sirro
0 Comments