Jeshi la Israel limeyashambulia maeneo mawili ya Gaza hii leo, baada ya ghasia zilizotokea jana katika eneo la mpaka na urushwaji wa maputo ya moto kusini mwa Israel.
Israel inadai imelishambulia eneo la kijeshi la Hamas linalotumika kutengeneza silaha na kutoa mafunzo pamoja na eneo la kuingia katika handaki karibu na Jabalia.
Kwenye taarifa yake, limesema mashambulizi hayo yalikuwa ni hatua ya ulipaji kisasi kwa Hamas kurusha maputo ya moto na makabiliano yaliyotokea jana Jumamosi.
Akizungumza mjini Washington alipokutana Rais Joe Biden, Waziri Mkuu wa Israel Naftali Bennett amesema Hamas, ambao wanatawala eneo la Gaza, wanawajibika kwa machafuko yoyote katika eneo la Wapalestina. Maandamano ya jana yalizuka huku Israel ikirusha gesi ya kutoa machozi na mabomu wakati Wapalestina wakichoma matairi katika mpaka wa Gaza na Israel.
0 Comments