MIFUGO SASA KUTAMBULIWA KIELEKTRONIKI


 Ng'ombe 6270 wametambuliwa kwa njia ya Kuvishwa Hereni za kielektroniki katika kijiji cha Kitosi Wilayani,Nkasi Mkoa wa Rukwa.

Akibainisha hayo kwenye Mkutano na wafugaji katika Kijiji cha Kitosi mara baada ya kushiriki katika zoezi la uwekaji hereni katika kijiji hicho Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mashimba Ndaki amesema zoezi la utambuaji wa Mifugo linatekelezwa nchini kote na kwa sasa wameanza na mikoa ya Mfano ambayo ni Rukwa ,Katavi , na Kigoma.

Amesema zoezi hili limeanza Katika kijiji cha Kitosi Wilaya ya Nkasi na tangu  lianze zaidi ya ng'ombe 6270 tayari wameshatambuliwa kwa kuvishwa hereni katika kijiji hicho.

Ameongeza kwa kusema zoezi hili nimuhimu kwa kuwa linaongeza thamani ya Mifugo ya wafugaji katika Masoko na kusaidia kufuatilia ubora wa mazao yanayo zalishwa na Mifugo iliyotambuliwa kwa njia ya hereni.

Mifugo itakayozalishwa itakidhi mahitaji ya soko la nje la Mifugo yetu na mazao yake.

Post a Comment

0 Comments