Kutokana na maelekezo ya Rais kwamba kodi ya miamala itazamwe upya ,kodi ile iliwekwa kwa mujibu wa sheria ya Bunge kwahiyo kuna namna ya kiuangalifu sana inatakiwa ifanyike bila kuvunja sheria ,tayari kamati iliyoundwa ikiongozwa na waziri wa fedha na mipango Mwigulu Nchemba na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Faustine Ndugulile ilifanya kazi ikawasilisha taarifa yake ya kwanza kwa waziri mkuu
''Waziri mkuu akaagiza marekebisho yakafanyike,marekebisho yamefanyika na taarifa itatolewa Agosti 31, 2021 kwahiyo mwisho wa mwezi huu itatolewa taarifa ya nini sasa serikali imeamua kuhusiana na namna ambavyo tutakwenda na tozo hii'' Gerson Msigwa Msemaji mkuu wa serikali
0 Comments