SITA WASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA KUWASHAMBULIA MAAFISA ARDHI MOROGORO

  


Kufuatia kutokea kwa tukio la wananchi kuchoma Moto Mali za Serikali ikiwemo  gari yenye namba za usajili  DFP 9402  pamoja pikipiki tatu ,kifaa Cha kupimia mipaka ya Shamba laptop 3,  Jeshi la Polisi Mkoani  Morogoro linawashikilia watu sita  wakituhumiwa kuhusika na tukio Hilo huku chanzo kikitajwa Kuwa ni mgogoro wa ardhi

Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro SACP Fortunatus Muslim amesema tukio hilo limetokea katika kijiji Cha Melela kata ya Chita wilaya ya Kilombero ambapo  watuhumiwa hao wamefanya tukio hilo mara baada ya maafisa ardhi kufika Katika Shamba linalomilikiwa mwekezaji  Daudi  Balal ( Marehemu) ambaye alikua Gavana wa benki kuu ya Tanzania kwa lengo la kupima mipaka 


Muslim amesema mwekezaji huyo alipewa Shamba hilo lenye Ukubwa wa Ekari Elfu mbili ambapo Mwaka  2001  wanakijiji walimpatia mwekezaji huyo Eneo hilo kwa  makubaliano ya kuwajengea Zahanati,Shule na kuwapatia huduma ya maji lakini hadi sasa mwekezaji huyo hakutekeleza makubaliano hayo  huku wananchi wakihitaji Shamba hilo kwa lengo la kufanya shughuli za maendeleo

Amesema Katika tukio Hilo mtu Mmoja amejeruhiwa ambaye ni dereva wa gari  Damas Sanga  miaka 51 baada ya Wananchi hao  kumkuta kwenye gari hilo kisha kumshambulia sehemu  mbalimbali za mwili wake.

Post a Comment

0 Comments