Jeshi la polisi limethibitisha kutokea kwa ajali katika eneo la Hanseketwa  - Old Vwawa  wilayani Mbozi mkoani Songwe ambayo imesababisha vifo vya wafanyakazi watano wa Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) kikosi kazi cha Fast Track  baada ya gari aina ya Land Cruser yenye namba za usajili T 8825 STL mali ya TRA  kugonga kwa nyuma Lori aina ya fuso yenye namba za usajili T 585ANE wakati wakifukuzana na gari iliyodhaniwa kubeba  magendo.

Ajali hiyo imetokea leo Agosti 23,2021 majira ya saa 11 alfajiri.