Mtandao wa Youtube umesema umeondoa kwenye mtandao wake zaidi ya video milioni moja za habari hatari za kupotosha kuhusu virusi vya corona, tangu kutokea kwa hilo mwaka iliyopita.

Taarifa hii inajiri wakati mitandao ya kijamii ikishutumiwa vikali na viongozi wa kisiasa kutokana na kushindwa kudhibiti usambazaji wa habari potofu kuhusu virusi vya corona pamoja na mada nyingine.

  Mtandao huo unaomilikiwa na kampuni ya Google katika taarifa kwenye blogi yake kwamba inategemea maelezo ya wataalamu wa afya, ikiwemo kituo cha kudhibiti magonjwa hapa Marekani (CDC) na shirika la afya duniani (WHO), lakini imekuta wakati mwingine kwamba, si rahisi kutambua habari potofu, wakati ukweli mpya unaibuka.

“Sera zetu zinaangazia kuondoa video za aina yoyote ambazo zinaweza kusababisha madhara mabaya kwa ulimwengu,” Ameandika ,afisa mkuu anaehusika na bidhaa'' Neal Mohan