Kamati ya maadili ya wabunge wa CCM imewaita kuwahoji  Wabunge watatu wa CCM Jerry Silaa (Ukonga), Askofu Josephat Gwajima (Kawe) na Humprey Polepole (mbunge wa kuteuliwa), leo Ijumaa Septemba 3, 2021.

polepolepic

Wabunge Jerry Silaa  na Josephat Gwajima wameitwa na kamati kwa agizo la Bunge,ambapo Bunge lilipitisha azimio la kuwasimamisha kutohudhuria mikutano miwili wakidaiwa kusema uongo na kushusha hadhi ya Bunge,  ingawa haikufahamika Polepole ameitwa kwa agizo la nani.

Baada ya mahojiano Polepole aliulizwa na waandishi wa habari kuhusu nini kilichojiri na hili ndilo jibu lake,"Utaratibu wa Chama chetu kikao cha Maadili ni kikao cha ndani kwahiyo taarifa zote zitatoka kwa utaratibu wa chama".

Mahojiano hayo yanafanyika Makao makuu ya CCM Dodoma na tayari wabunge hao wote wameshafika.

polepoleepiccc