Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akivalishwa Mavazi ya Kimila kuwa Chifu Mkuu wa Machifu wote Tanzania na kuitwa jina la Hangaya yani ni Nyota inayong`aa, katika Tamasha la Utamaduni (Mila na Desturi zetu) lililofanyika leo Sept,08,2021 katika Viwanja vya Redcross Kisesa Magu, Mkoani Mwanza.
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa ameshikilia mkuki na ngao ikiwa ni ishara ya kupewa madaraka ya kuwa Mkuu wa Machifu nchini wakati mara baada ya kufunga Tamasha la Utamaduni leo Septemba 08, 2021 Kisesa wilaya ya Magu mkoani Mwanza ambalo limeandaliwa na Umoja wa Machifu Tanzania (UMT) lenye lengo la kulinda mila na desturi za mtanzania lililoongozwa na kaulimbiu ya “Turithishe Utamaduni Wetu, Tudumishe Utamaduni Wetu, Amani na Umoja ni Tunu Zetu.” |
0 Comments