![]() |
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini Benaya Kapinga akichangia shilingi Laki tatu (300,000) kwaajili ya kuunga jitihada za maendeleo katika ujenzi wa Kigango cha Langiro parokia ya Kipapa. |
Mbunge Benaya akitoa salamu za Jumapili kwa waumini hao amesema Wananchi wengi wanashindwa kupatiwa matibabu stahiki ni kwa sababu ya kukosa bima za Afya jambo ambalo hupelekea baadhi yao kuugulia majumbani na mwisho wanaweza kupoteza maisha.
Benaya ambaye alishiriki ibada na waumini hao ambayo iliongozwa na paroko wa parokia hiyo Fr, Ngahy amesema kuwa ni vema waumini hao wakaenda kuwaambia na Wananchi wengine namna ya umuhimu wa kuwa na bima za Afya.
![]() |
Mbunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini Benaya Kapinga akiwa na baadhi ya Viongozi wa parokia ya Litembo akiwemo Paroko Fr, Ngahy muda mfupi baada ya mbunge huyo kushiriki misa takatifu kwenye parokia hiyo. |
Aidha mbunge huyo licha ya kuwaambia umuhimu wa bima za Afya kwa waumini hao lakini bado amewaambia wajiandae na kuhesabiwa sensa itakayofanyika mwakani 2022 ili kupata idadi sahihi ya Wananchi wa Jimbo hilo pamoja na Nchi nzima.
Amesema kuwa baadhi ya Wananchi wamekuwa wakibeza suala la sensa jambo ambalo hupelekea kutokuwa na takwimu sahihi ya Wananchi wanaotakiwa kupatiwa huduma za maendeleo wakati wa kupitisha bajeti ya taifa kule bungeni.
Hata hivyo mbunge huyo amepokea kero mbalimbali za waumini hao na Wananchi kwa ujumla huku akiahidi kwenda kuzifanyia kazi ili ziweze kupatiwa ufumbuzi.
Pia Mbunge huyo ambaye ametoa salamu hizo katika makanisa mawili ya Litembo pamoja Kigango cha Langiro ,licha ya kupokea changamoto hizo na kuahidi kuzitafutia ufumbuzi lakini amechangia shilingi Laki tatu (300,000.) kwaajili ya ununuzi wa kinanda katika Kigango cha Langiro wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa pamoja na ununuzi wa kinanda.
0 Comments