TIMU ya Yanga imepoteza mchezo wake wa ligi ya Mabingwa Afrika Dhidi ya Rivers United kwa bao 1-0 mchezo uliochezwa leo Septemba 12, kwenye uwanja wa Mkapa jijini Dar es salaam.
Goli pekee limefungwa na mshambuliaji Moses dakika 52, ya mchezo akiunganisha pasi safi baada ya kupigwa kona fupi.
Yanga sasa ina mtihani mzito wa kuhakikisha inaibuka na ushindi ugenini nchini Nigeria ili kufuzu kwa mzunguko wa pili.
0 Comments