Mwanamke mmoja Mkazi wa mtaa wa Mtwivila B ,Manispaa ya Iringa aliyefahamika kwa jina la Rehema Ismail amekutwa amefariki na mwili wake ukiwa umetelekezwa  kando ya barabara inayounganisha mitaa ya Mtwivila B na Mtwivila C mkoani Iringa.

Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Mtendaji wa kata ya Mtwivila Thadei Mhanga, amesema alipokea taarifa ya tukio hilo mnamo majira ya saa mbili asubuhi  leo oktoba 29,2021.

Jeshi la polisi Manispaa ya Iringa limefika katika eneo la tukio na kuchukua mwili kwaajili ya uchunguzi zaidi.