Mohamed Said Issa wa chama cha ACT Wazalendo ametangazwa kuwa mshindi wa uchaguzi mdogo wa jimbo la Konde -Kaskazini Pemba kwa kupata kura 2391.
Katika matokeo hayo Issa amefuatiwa na mgombea wa CCM Mbarouk Amour Habib aliyepata kura 794 kati ya kura 3338 zilizopigwa.