Katika hotuba kupitia televisheni Burhan amesema kwamba nchi nzima ilikuwa imesimama kutokana na upinzani wa kisiasa.
Ameongeza kusema kwamba uzoefu ulionekana katika kipindi cha miaka miwili iliyopita umethibitisha pande za kisiasa zilisababisha kutokuwepo na maelewano katika kipindi cha mpito.
Vilevile jenerali huyo ameeleza kwamba, waziri mkuu Abdalla Hamdok, alikuwa nyumbani kwake siku moja baada ya kuripotiwa kwamba ameshikiliwa na wanajeshi wakati wa mapinduzi.
Ameongeza kusema kuwa waziri mkuu Hamdok yupo na afya njema na atarejea nyumbani baada ya hali ya mambo kutulia.
Source:VOA
0 Comments