Mwalimu Mkuu wa shule ya Msingi Mkuyuni aliyefahamika kwa majina ya Mussa Basila (46) ,Tarafa ya Mkuyuni Morogoro vijijini anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za kumpiga hadi kumng'oa jino la juu Mwalimu mwenzake, Witness Makoti (31) huku chanzo kikiwa bado hakijulikani.
Kamanda wa Polisi Morogoro, Fortunatus Musilimu ametbibitisha kushikiliwa Kwa mtuhumiwa huku akisema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 15 mwaka huu shuleni hapo ambapo mtuhumiwa alimpiga kwa kutumia Fimbo, Ngumi na kumshambulia sehemu mbalimbali za mwili.
0 Comments