Vidonda vya tumbo ni moja ya shambulio idadi kubwa ya watu wakiwemo wanafunzi na wafanyakazi maofisini.

Leo nimeamua kudokeza kidogo kuhusu baadhi ya matunda ambayo huzuia na kusaidia kuondokana na tatizo la vidonda vya tumbo.

Baadhi ya matunda hayo ni 

MATANGO

Ulaji wa matango kwa wingi husaidia kuondoa tatizo hilo kwa kulifanya tunda kuwa sehemu ya mlo wako kila siku.


MAPARACHICHI

Tunda hili pia hufanya kazi sawa pamoja na tango katika kupambana na tatizo hilo.


KOMAMANGA

Tunda hili pia husaidia katika kuondoa tatizo hili . Chukua mbegu za Komamanga kisha changanya na asali halafu tumia vijiko viwili vya chakula kwa siku yaani asubuhi kijiko kimoja na jioni vivyo hivyo kwa muda wa siku 21.



Licha ya matunda hayo pia unashauriwa kunywa maji mengi kila siku angalau lita 2 kwa siku ili kuepuka vidonda vya tumbo kwa mujibu wa wataalamu.