Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto kupitia kwa Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-Afya Bi. Catherine Sungura imewataka wananchi kuwa watulivu kufuatia video inayozunguka mitandaoni kuhusu mgonjwa aliyefika Hospitali ya Mkoa wa Temeke kudai hakupata huduma stahiki huku watumishi wakiendelea na shughuli binafsi.
"Wizara ya Afya imepokea na kusikiliza video inayozunguka mitandaoni kuhusu mgonjwa aliyefika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, Jijini Dar es Salaam kudai hakupata huduma stahiki huku watumishi wakiendelea na shughuli binafsi.
"Wizara imetoa maelekezo kwa Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam afuatilie na kuwasilisha taarifa. Tunaomba wananchi wawe watulivu wakati jambo hili likifanyiwa kazi." Ilieleza taarifa hiyo.
"Aidha, Wizara inaomba kupata mawasiliano ya mgonjwa au ndugu wa mgonjwa huyo aliyelalamika Ili kurahisisha ufuatiliaji wa kina na kumpata mlalamikaji." Ilimalizia taarifa hiyo.
0 Comments