Vijana wa kituo cha Kangaa Herbal Clinic wakiwaonyesha wakazi wa Songea Mkoani Ruvuma namna ya kuchanganya mimea ambayo inayoweza kutibu magonjwa mbalimbali.
Na.Amon Mtega ,SONGEA.
VIJANA wajasiriamali wanaojishughulisha na uuzaji wa dawa za tiba mbadala kutoka katika kituo cha Kangaa Herbal Clinic kilichopo Wilaya ya Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wametoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa Songea ya namna ya kuzilinda Afya zao kupitia mimea(Matunda) iliyopo hapa Nchini.
Bashir Mbwana mmoja wa Vijana hao Wajasiriamali akitoa maelekezo ya namna ya matumizi ya mimea juu ya kulinda Afya ya mwanadamu amesema watu wengi wamekuwa wakishindwa kutambua mimea iliyopo ni tiba bora kwa mwanadamu jambo ambalo limekuwa likiwasababishia kuendelea kuishi na magonjwa.
Akitoa maelezo hayo kupitia mchanganyiko wa mimea mbalimbali ikiwemo ya vyakula kwenye siku ya maonyesho ya biashara zinazoibuliwa na wanawake wajasiriamali wa Mkoa wa Ruvuma (Tanzania Women Chamber Of Cmmerce) yaliofanyika Manispaa ya Songea Mkoani humo,kijana huyo amesema kuwa kama watu watazingatia matumizi sahihi ya mimea iliyopo basi wengi wao wataepukana na magonjwa mbalimbali.
Naye Evarist Siriwa amesema kuwa watu wengi wanaokuwa wamefanikisha kupatiwa maelezo ya matumizi sahihi ya mimea hiyo wamekuwa wakipata matokeo mazuri kwenye Afya zao jambo ambalo linawafanya waendele na shughuli za uzalishaji kwenye jamii.
Siriwa amesema kuwa mimea inayotumika wengi wao wanayo majumbani mwao ila ni elimu tu ya utambuzi juu ya faida za mimea hiyo .
Vijana hao wamekuwa na uwigo mpana mkoani Ruvuma kufuatia Clinic hiyo kujikita katika matamasha mbalimbali ambapo banda lao limekuwa kimbilio la watu wengi kwenda kupatiwa maelezo juu ya matumizi ya mimea hiyo ambayo asilimia kubwa ni matunda .
Katibu tawala msaidizi wa mkoa wa Ruvuma Bakari Mketo aliyekuwa mgeni rasmi siku ya ufunguzi wa maonyesho hayo akiwa kwenye banda la Vijana hao amewapongeza Vijana hao kutoa elimu ya kutosha huku akiwataka baadhi ya wanachi ambao hawana elimu hiyo waweze kujifunza.
0 Comments