WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi maafisa mapato watatu wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa na kuiagiza Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Jeshi la Polisi kuwachunguza na kuwafikisha katika vyombo vya sheria.

“Hatuwezi kuwa na watumishi wa umma walioaminiwa na Mheshimiwa Rais amewaleta hapa Kilwa kuwatumikia wananchi mkusanye mapato yakajenge zahanati, shule na visima vya ninyi mnakula tu, haiwezekani, sasa nawasimamisha kazi, Polisi na TAKURURU nendeni mkawachunguze na kuwafikisha mahakamani”

Waziri Mkuu amewasimamisha kazi watumishi hao Jumatano, Oktoba 6, 2021 wakati akizungumza na madiwani, watumishi na wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa akiwa kwenye ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika mkoa wa Lindi.

Watumishi waliosimamishwa kazi ni Bahaye Shilungushella, Ally Kijonjo na Mohamed Samodu.