AMUUA BINTI YAKE BAADA YA KUKATAA KUOLEWA



Jeshi la Polisi Mkoani Kigoma linawashikilia ndugu watatu wa familia Moja Kwa kumpiga Hadi kumuua Binti wa miaka 17 aliyejulikana Kwa jina la Mbaru Juakali mkazi wa Lufugu wilayani Uvinza Kwa kukataa kuolewa Kwa ahadi ya mahari ya Ng'ombe 13.

Akithibitisha kutokea Kwa tukio hilo kamanda wa Polisi Mkoani Kigoma ACP James Manyama amesema tukio hilo limetokea Jumatano Novemba 10,2021 ambapo Binti huyo alipigwa sehemu mbalimbali za mwili wake Kwa fimbo wakimlazimisha kuolewa bila ridhaa yake.

Kamanda Manyama amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Kulwa Juakali(40),mkulima na mkazi wa Lufugu ambaye ni baba mzazi ,Shija Juakali (44), mkulima na mkazi wa Lufugu ambaye ni baba mkubwa na Majiba Juakali (29), mkulima na mkazi wa Lufugu ambaye ni baba mdogo wa Binti huyo.

Jeshi la Polisi Mkoani humo linaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na utakapokamilika watuhumiwa hao watafikishwa mahakamani Kwa hatua za kisheria zaidi.

Post a Comment

0 Comments