ASHIKILIWA KWA KUKUTWA NA NYARA ZA SERIKALI


JESHI la Polisi linamshikilia mtu mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa kwa tuhuma za kukutwa na meno mawili ya tembo.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Mjini Kibaha kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa amesema kuwa mtuhumiwa huyo anashikiliwa kwa mahojiano zaidi.


Mtuhumiwa huyo alikamatwa wilayani Bagamoyo atafikishwa mahakamani upelelezi utakapokamilika ambapo jeshi la polisi watashirikiana na ofisi ya wanyamapori kujua thamani ya meno hayo.

Katika tukio lingine Jeshi hilo limekamata mabegi yaliyokuwa yakisafirishwa kama mizigo yakiwa yamejaa bhangi kilo 172, kete 272 na puli 13.

Post a Comment

0 Comments