MPE FURAHA JAPO KIDOGO


Hakuna anayependa huzuni imfike,kila MTU anapenda kuwa na furaha na Amani moyoni  bila kujali maisha na uchumi wake. 

MAHUSIANO na NDOA nyingi Leo hakuna furaha sababu ya mmoja kushindwa kutimiza wajibu wake.

Mwanaume ukimpata mwanamke mwenye upendo wa dhati ambae hakukupendea PESA na Mali zako basi jua anahitaji sana uwepo wako kuliko PESA zako. Unaweza MPA kila kitu na kiasi chochote cha PESA ,lakini ukiwa mbali nae kimwili na hisia ni shida.

UBIZE uliopitiliza kiasi kwamba ukirudi huna muda na mwanamke hilo ni tatizo pia. Inafika kipindi kwa mwezi unalala nae Mara 2 tu tena za kichovu ila kila Mara mpo wote.

PESA zako zisikufanye ujione umemfunga mwanamke wako,  nae anaweza tafuta zake. Nae ni binadamu ana hisia MPE muda wako,MPE penzi lako tena mkoleze ipasavyo.

Tenga muda wa kuwa na familia yako katika harakati zako za utafutaji.

Kuna wanawake wameolewa na wanaume mwenye PESA kila kitu wanapewa ila hawana furaha maana mwanaume akili yote ni PESA mke kasahaulika,anaishi kama mjane.

Kuna wadada mwenye PESA na magari ya kutembelea ila ni wapweke sana mioyoni mwao maana hawapati kile wanachopata wengine

Tenga mda wa kufurahi nae

Tenga mda kushinda na watoto

Kulipia tu Ada huku hujui umri wala darasa alilopo mtoto ni shida

Post a Comment

0 Comments