Tunatambua kuwa mwanamke anafanya kazi kubwa sana ambayo lau kama ingekuwa ni kampuni basi pangehitajika watu zaidi ya 10 kuzifanya... atamtunza mume, watoto, nyumba na familia kwa ujumla...
Wakati fulani mume anaweza akampuuza na asimthamini, licha ya kujitoa kwa moyo wote kumtunza na kuihudumia familia... Hivyo, kutotoa kipaumbele kwa mke ni kosa kubwa ambalo linaweza likamgharimu mume... mke akipata mtu anayempa kipaumbele na kumuonesha thamani hakika hataacha kuitumia hiyo fursa.
2.UKOSEFU WA MAHABA.
Kwa asili mwanamke anatakiwa kupendwa... Mwanamke anahitaji kupendwa... mwanaume yeye ana asili ya kupenda ngono tu ukimpa ngono basi, anaridhika lakini mwanamke anahitaji kubembelezwa, kudekezwa, anahitaji aambiwe maneno maneno matamu,Hivyo hayo yanapokesana ni rahisi sana kushawishika kusaliti kwa mwingine anayemjali zaidi.
3.UKIMUONESHA USALITI.
Miongoni mwa mambo ambayo huibadilisha roho ya mwanamke ni pale anapogundua kuwa mumewe kipenzi anamsaliti,Hapo mwanamke anaweza akabadilika kabisa,Wapo wanaosamehe, lakini wapo wanaolipiza kisasi inategemea na imani yake.
4.KUTOJIAMINI
Mwanamke anahitaji mwanaume anayemfanya ajiamini,Iwapo mwanaume hatekelezi jukumu hilo, akimpata mtu anayemfanya ajiamini, yanaweza kutokea mengine kabisa,Hivyo ni muhimu kujifunza na kujua namna sahihi ya kuishi na mwanamke na hata likitokea tatizo ujitathimini unapokesa na kujirekebisha.
TAMBUA:
Makosa mengi ya wanawake katika mahusiano/Ndoa kwa 98% huzalishwa na Mwanaume mwenyewe hutaki kukubali unakosea na ukabadilika unaishi kwa mazoea kukitoa tatizo unamtafuta mchawi wakati unakuta shida imeanzia kwako
0 Comments