NA AMON MTEGA,SONGEA.
JUMUIYA ya Wanawake wa Chama Cha Mapinduzi CCM (UWT) wa Songea Vijijini na Songea Mjini Mkoani Ruvuma wamempongeza mbunge wa Viti maalumu wa mkoa huo Jacqueline Ngonyani (Msongozi) kwa kuendelea kuzitekeleza ahadi mbalimbali alizoziahidi kwao.
Pongezi hizo wamezitoa wakati wa vikao vya mabaraza ya wanawake wa CCM ambavyo vilikaliwa kwa awamu tofauti ambapo lilianza baraza la wanawake Songea Vijijini na kisha baraza la wanawake wa Songea mjini ambapo mbunge Jacqueline Ngonyani alihudhuria mabaraza hayo kisha kuendeleza kukamilisha ahadi alizoziahidi .
Baadhi ya Wanawake wa Jumuiya ya UWT ya CCM Wilaya ya Songea Mjini wakimsikiliza Mbunge wa Viti maalum Jacqueline Ngonyani (Msongozi)wakati wa kikao cha baraza hilo. |
Baadhi ya ahadi ambazo anazitekeleza kwa wanawake hao ni pamoja ugawaji wa mbegu za Alizeti zenye ujazo wa kilo mbili ambazo hutumika kwa hekari moja ,ugawaji wa majiko ya gesi ikiwa ni sehemu ya kupambana na uharibifu wa mazingira .
Akizungumza mwenyekiti wa Jumuiya ya wanawake Wilaya ya Songea Mjini Imelda Njelekela amesema mbunge huyo amekuwa akitekeleza ahadi ambazo amekuwa akiwaahidi wanawake hao wakati wa uchaguzi .
Njelekela amesema kuwa mbunge huyo licha ya kutoa mbegu za alizeti pamoja na majiko ya gesi lakini bado amewapatia wanawake wa kwenye Jumuiya chupa za chai ,Charahani kwa kila mwanajumuiya kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa pamoja na saa za mkononi .
Kwa upande wake mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Songea Vijijini Nelly Duwe akiwa kwenye baraza la wanawake wa Songea Vijijini amewataka wanawake kuendelea kumuunga mkono mbunge huyo ili aweze kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Ruvuma Jacqueline Ngonyani (Msongozi)akiwaonyesha wanawake wa CCM Wilaya ya Songea Vijijini namna ya kulitumia jiko la gesi. |
Naye mmoja wa wanawake hao ambaye ni katibu wa Jumuiya hiyo kata Mletele Flora Mkanula amesema kuwa msaada waliopewa wa mbegu za Alizeti pamoja na majiko ya gesi itasaidia kuibadilisha jamii kuwa na uelewa hasa wakutumia mazao mbadala badala ya kung’ang’ania zao moja la mahindi na kuwa jiko la gesi litasaidia kuionyesha jamii kuwa inaweza ikakabiliana na janga la uharibifu wa mazingira kwa kutumia gesi badala ya kuni na mkaa.
Mbunge wa Viti maalum Mkoani Ruvuma Jacqueline Ngonyani (Msongozi) akizungumza na wanawake wa CCM Wilaya ya Songea Mjini kwenye mkutano wa baraza la UWT . |
Mbunge wa Viti maalum Jacqliene Ngonyani amesema kuwa anatambua kazi zinazofanywa na wanawake hao hivyo ataendelea kuwa nao bega kwa bega ili mwisho wa siku kila mwanamke aweze kujikwamua kiuchumi .
0 Comments