FANYA HAYA KUDUMISHA MAHUSIANO YAKO



Mawasiliano yana nguvu ya kujenga au kubomoa mahusiano au ndoa kwa waliopo mbali mbali.

Mawasiliano imara yaani ya Mara kwa Mara hufanya muwe karibu kifikra , yaani kujuliana hali iwe kwa SMS au kuongea kwa simu. Huwa imara zaidi kila mmoja anapo pata nafasi amkumbuke mwenzake na kumjulia hali

Mawasiliano hafifu ni sumu, unakuta Kuanzia asubuhi hadi usiku hujapata simu wala SMS kutoka kwa MTU wako na wala wewe hujamtafuta,wengine inaweza pita hata siku 3 au wiki hata mwezi.

Mbaya zaidi mawasiliano ya upande 1, yaani unakuta MTU mmoja yeye ndiye kila Mara anamtafuta mwenzake iwe kwa SMS au kupiga huku Mwenzake kazi yake ni kujibu na mda mwingine hajibu.

Mawasiliano ya Mara kwa Mara yanaweza kuwafanya watu kuwa marafiki na hatimaye kuwa wapenzi , maana kila MTU anapenda kupata faraja na sehemu ya kupeana mawazo ya kimaisha.

Atasema yupo bize,anachoka na kazi,hana salio ila mtandaoni unamuona yupo online na ana post status ila hana mda nawe,kuna mda simu yake bize ila kwako haongei.

Ukiona mawasiliano yamepungua tambua ni upendo ulio pungua, Kuendelea kujipendekeza kutaka mawasiliano yawe kama mwanzo ni kutafuta maumivu.

MTU hata kama yupo bize vipi hawezi kukosa sekunde hata kukutumia SMS .

Usilazimishe abaki kwako wakati kafikiria kuondoka,

Post a Comment

0 Comments