Watu wawili wamefariki dunia na wengine 25 kujeruhiwa baada ya basi la kampuni ya SEA kugongana na lori katika kijiji cha Unyenye Wilayani Mlele Mkoa wa Katavi.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema ajali hiyo imesababishwa na mwendokasi na uzembe wa dereva wa basi ambaye alikuwa akifukuzana na madereva wenzake wa mabasi mengine mawili yaliyokuwa katika msafara mmoja yakitokea katika stendi ya Majimoto mkoani humo.
Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo Kamanda wa polisi mkoa wa Katavi Benjamini Kuzaga amesema taarifa zaidi zitatolewa kuhusu ajali hiyo huku mganga mkuu wa Halmashauri ya Mpimbwe ,Martine Lohay akithibitisha kupokea majeruhi 25 na miili miwili ya watu waliofariki kutokana na ajali hiyo.
0 Comments