Mchambuzi nguli wa masuala ya soka nchini Mwalimu Alex Kashasha amefariki dunia kwa tatizo la figo ambalo lilipelekea kulazwa katika hospitali ya Kairuki jijini Dar es salaam mpaka umauti unamkuta agosti 19/2021 alikuwa akipatiwa matibabu hospitalini hapo.
Mwalimu Kashasha aliucheza mpira wa miguu akiwa shuleni, chuo cha Ualimu Butimba na aliweza kufundisha mpira wa miguu katika timu mbalimbali kama Majimaji ya Songea kwa kipindi kifupi, timu ya Maji Mara, timu ya Mkoa wa Mara wakati wa mashindano ya Taifa CUP.
Kabla ya umauti kumkuta alikuwa akifanya kazi na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) pia alikuwa mchambuzi wa gazeti la Mwanaspoti Jumamosi.
Mwalimu Kashasha ameacha mjane na watoto wawili wa kike.
Kwa hakika kifo chake ni msiba mkubwa kwa wadau wa soka na familia kwa ujumla.
Bwana ametoa na Bwana ametwaa Jina lake lihimidiwe apumzike kwa Amani
Amina.
0 Comments