ALIYEMBAKA MSICHANA WA KAZI KUFIKISHWA MAHAKAMANI AGOSTI 31,2021



Katika juhudi za kukomesha Ubakaji na udhalilishaji visiwani Zanzibar hatimaye Mshtakiwa Sadalla Juma Sadalla mwenye umri wa miaka 74 mkazi wa  Bububu,Unguja,atafikishwa mahakamani Vuga,Unguja siku ya jumatatu 31 Augosti 2021 kwa makosa ya kumbaka msichana wake wa kazi mwenye umri wa miaka 15 (jina limehifadhiwa). 

Sadalla alifikishwa mahakamani siku ya 18 Augosti 2021 na kusomewa mashtaka yake na kesi hiyo imepangiwa tena tarehe 31 Augosti 2021 katika mahakama ya Vuga mjini Unguja. 

Mshtakiwa huyo alilalamikiwa na wanaharakati visiwani Zanzibar kuwa ni mzoefu katika vitendo vya ubakaji pamoja na udhalilishaji na alipombaka msichana wake wa kazi mwenye umri wa miaka 15 ,alikuwa yupo huru  na alipanga kuondoka unguja kukimbia kesi lakini vyombo vya usalama viliwahi kumshika na hatimaye kumpeleka mahakamani

Mzee Sadalla yupo mahabusu kwa kuwa shitaka la kubaka,udhalilishaji halina dhamana.

Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inayoongozwa na Mheshimiwa Rais Dkt.Hussein Ally Mwinyi imepania kukomesha vitendo vyote vya Ubakaji na udhalilishaji,pamoja na madawa ya kulevya vinakoma kabisa visiwani Zanzibar.


Post a Comment

0 Comments