Mwenyekiti wa kamati ya maadili na madaraka ya Bunge Emmanuel Mwakasapa ameomba kibali cha spika wa bunge cha kukamatwa kwa mbunge wa jimbo la Ukonga Jerry Silaa na kupelekwa mbele ya kamati kesho saa nne kutokana na kutofika mbele ya kamati leo saa tano kama ilivyokuw a imepangwa .

Mwakasaka amesema Mbunge Jerry Silaa hakutoa taarifa za kutofika kwake na kwamba kamati imemsubiri hadi saa naane mchana lakini hakutokea .

Jerry Silaa alifika bungeni agosti 24,2021 kuitika wito wa uliomtaka afike mbele ya kamati ya maadili na madaraka ya bunge kujibu tuhuma mablimbali zinazomkabili ikiwemo ya kusema uongo na kushusha hadhi na  heshima ya bunge ambapo mahojiano hayo yalitarajiwa kuendelea tena leo .