BAADA YA CHAMA KUUZWA MANARA AFUNGUKA



Baada ya Ezekiel Kamwaga afisa habari wa klabu ya Simba kuthibitisha kumuuza mchezaji Clatous Chota Chama kwa miamba ya soka Morocco,Berkane RBS aliyekuwa msemaji wa klabu hiyo Haji Manara ameibuka na kusema yafuayo,

''Niliiona miguu yako siku ya kwanza nilipagawa na ufundi wako.. Nakumbuka tukiwa Kitwe Zambia,Picha hiyo ya mbele ikatawala katika Mitandao na magazeti ya kwenu. 

Nakumbuka pia wakati tunarudi ukaniambia tutafuzu kwenye mechi ya marudiano,ahhhh Mwamba ukafunga goli maridadi mno dhidi ya Nkana. 

Real friend na jirani yangu nikutakie kheri nyingi katika maisha mapya Morocco na naamini utafanikiwa 

Nani aliniamini nilipokuita Mwamba wa Lusaka 2018? Hakika Tanzania ilishuhudia talent murua kwa miaka mitatu itoshe kusema nitakumiss sana my hero''

Post a Comment

0 Comments