Baada ya Emmanuel Mwakasaka Mwenyekiti wa kamati ya Bunge ya Maadili ,Haki na Madaraka ya Bunge kutoa ripoti kuhusu hatia walizokutwa nazo wabunge Jerry Silaa wa Ukonga na Josephat Gwajima wa Kawe Spika wa Bunge Job Ndugai amemtoa Bungeni Mbunge Jerry Silaa.
"Gwajima hayupo,Silaa Yupo sasa naomba utoke nje tutaonana January 2022 na Sajenti naomba mtoke nae nje ya viunga vya Bunge na katika kipindi hiki ambacho wamesimamishwa hawatoruhusiwa kukanyaga maeneo ya Bunge isipokuwa kwa ridhaa ya Spika na watapata nusu ya mshahara na nusu ya mambo mengine ambayo wanastahili kuyapata hivyo ndivyo kanuni zinavyosema" Spika Job Ndugai
0 Comments