Kamati ya Bunge ya Haki ,Maadili na Madaraka ya Bunge leo bungeni imetoa ripoti ya shauri la mbunge wa Kawe ,Josephat Gwajima kupewa adhabu ya kutokuhudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge.

"Kamati imebaini kauli za Mh. Gwajima zinadhalilisha nafasi ya Mbunge na kushusha heshima ya Bunge ,wabunge na viongozi,zinachonganisha mhimili wa bunge dhidi ya Serikali na wanannchi ,zinaonyesha dharau na kushusha heshima ya Bunge na uongozi wa Bunge " Mwenyekiti wa kamati Emmanuel mwakasaka.

Aidha kamati ya Bunge imetoa maoni kuwa , "Vyombo vya kisheria vifuatilie mwenendo na vitendo vya askofu Gwajima kutokana na kauli mbalimbali alizotoa kwani vinaashiria uvunjifu wa amani   na usalama wa nchi na kuwepo kwa jinai".

''Pia suala hili lishughulikiwe kwa mujibu wa sheria na maadili ya umma ,lifikishwe kwenye chama anachotoka ili aweze kuchukuliwa hatua kwa mujibu wa kanuni za chama chake'' Mwakasaka 

Mwakasaka amesema wakati akisoma taarifa yake kuwa shahidi alikiri kuwa kauli zote ni za kwake na akasema ni mahubiri--" Niliyasema nikiwa kanisani na ninayasema nikiwa kama Askofu ,kosa kubwa ni kujaribu kuyakosoa mahubiri, huwezi ku-question mahubiri, Kamati ilijiridhisha kuwa mahubiri yanayotolea yanapaswa kuzingatia sheria za nchi hivyo kauli zinazotolewa haziwezi kuwa na kinga ya kuhojiwa"

Gwajima alishindwa kuthibitisha kauli zake na hana kielelezo chochote kama alivyowaaminisha wananchi ,sala la kupewa rushwa hakutoa ushahidi wowote 

Askofu Gwajima hakukiri wala kujutia makosa yake hivyo kamati kumtia hatiani na makosa hayo

Hivyo basi bunge linaazimia Mheshimiwa Mbunge wa Kawe apewe adhabu ya kutohudhuria mikutano miwili mfululizo ya Bunge baada ya kupitishwa kwa azimio hili.

kwa mujibu wa Mwakasaka Askofu Gwajima alifanya makosa hayo kati ya tarehe 25 julai ,01 Agosti,15 Agosti na 21 Agosti.