Mwili wa Hamza Mohamed ambaye alifariki dunia katika majibizano ya risasi kati yake na polisi hatimae umezikwa  katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam majira ya saa 2:30 usiku .

Kwa mujibu wa msemaji wa familia ya Hamza ,Abdulrahm Hassan amesema Mazishi yalitarajiwa kufanyika mchana saa saba lakini haikuwa hivyo kwa sababu ya kazi ya kutoa risasi zilizokwama .

Mwili huyo ulizikwa baada ya kuswaliwa katika msikiti wa Mamuur uliopo Upanga jijini Dar es salaam.