Waziri wa afya ,maendeleo ya jamii,jinsia ,wazee na watoto Dkt. Doroth Gwajima ameliagiza jeshi la polisi na Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU kumkamata na kumuhoji mbunge wa jimbo la Kawe askofu Josephat Gwajima ili aweze kuthibitisha kauli ambazo anazitoa dhidi ya serikali na viongozi kuhusu chanjo ya Uviko19.
Ametoa agizo hilo leo Agosti 17,2021 akiwa katika kijiji cha Kyatunge wilayani Butiama na kubainisha kuwa askofu Gwajima kwa makusudi amekuwa akitoa taarifa za kupotosha jambo ambalo linaivuruga wizara yake na serikali katika suala zima la mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Ameongeza kuwa amekuwa akisisitiza kuwa hatakubali lupatiwa chanjo hiyo na kuwataka waumini wake kutojitokeza kwenda kupata chanjo ya kukabiliana na Uviko-19
0 Comments