Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri Wilaya ya Gairo  Asajile Mwambambale ambaye alishikiliwa na jeshi la polisi mkoa wa Morogoro kwa tuhuma za Wizi Mabati 1172 Mali ya Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa amefunguka mwanzo mwisho Kuhusu Wizi huo.

Asajile Mwambambale ambaye alikua mkurugenzi Wilaya ya Kilosa Kabla ya Rais Samia Kufanya mabadiliko ya wakurugenzi Hivi karibuni na  kumuhamishia Wilaya ya Gairo ambapo hivi karibuni alishikiliwa na polisi kwa madai ya kuhusika na  Wizi wa Mabati 1172 akishirikiana na watumishi wengine Saba wa Halmashauri hiyo ya Kilosa Kabla ya kuhamishwa .

Mwambambale amesema Wizi huo umetokea  agosti 17 Mwaka Huu wakati tayari akiwa amehamishiwa Wilaya ya Gairo na sio juni 17 Mwaka huu kama taarifa ilivyotolewa.

TAZAMA VIDEO HII KWA TAARIFA ZAIDI