Mkuu wa wilaya ya Moshi Said Mtanda


Mkuu wa wilaya ya Moshi Said Mtanda  amefika katika shule ya Sekondari Rau kutoa pole kwa wanafunzi  na uongozi kufuatia tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa kidato cha nne Joackim Sanga aliyeuawa kwa kuchomwa kisu na  anayedaiwa kuwa ni mhitimu wa Rau sekondari mwaka 2020 wakati wakiwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu kati ya shule ya sekondari Rau na Karanga agosti 20..

Pia ametoa maagizo kwa jeshi la polisi kuhakikisha linamsaka na kumkamata na kumfikisha kwenye vyombo vya sheria  mtuhumiwa wa mauaji hayo .