Jeshi la polisi jijini Dar es salaam limethibisha kuwa askari wawili wameuawa kwa kupigwa risasi na mtu ambaye hajafahamika jina aliyekuwa akirusha risasi ovyo karibu na Ubalozi wa Ufaransa

.

Katika tukio hilo pia mtu ambaye hajajulikana jina lake ni mmoja kati ya waliouawa huku wengine sita wakijeruhiwa .

Tukio hilo limetokea leo jijini humo huku aliyetekeleza tukio hilo nae akiuawa na polisi wakati wa majibizano ya risasi.