Kushoto ni Waziri wa Afya Dkt.Doroth Gwajima na Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima
''Askofu Gwajima ni mtumishi wa Mungu na Serikali pia imetoka kwa Mungu ,cha msingi ni kuangalia kwa nini hii vita inakuwepo kati ya Gwajima na serikali au shetani ndiyo yupo hapa katikati " Rose Muhando
Ameongeza pia " Viongozi wa Serikali wanamuhitaji Mungu na viongozi wa makanisa wanahitaji Serikali ,cha kuangalia ni kweli Askofu Gwajima anagombana na Dkt.Gwajima au kuna nini hapa kati,cha kuzingatia ni kwamba tunapigana na muovu hatupigani na Waziri wa afya wala mchungaji".
"Tunaihitaji serikali pia tunahitaji viongozi wetu wa dini ,cha msingi tukae pamoja hili jambo lililotokea lisilete mtafaruku ,sisi sote ni watoto wa hapa nyumbani tusimpe Ibilisi nafasi". Amemalizia Rose Muhando.
0 Comments