Jeshi la polisi mkoani Morogoro linawashikilia watu Saba  akiwemo aliyekua Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilosa Asajile Mwambambale ambae kwa Sasa amehamishiwa Wilaya ya Gairo na wengine sita ambao ni  watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Kilosa Kwa wizi wa Mabati 1172.

Akizungumza na Waandishi wa habari Kamanda wa polisi mkoa wa Morogoro  SACP Fortunatus Muslim  amesema tukio Hilo limetokea Juni 17 Mwaka Huu ambapo watuhumiwa hao wanadaiwa kuiba Mabati hayo Kwenye stoo ya halmashauri hiyo Huku milango ikiwa haijavunjwa


Amesema Mkurugenzi Huyo kwa kushirikiana na watumishi wa kutoka idara ya ugavi watatu  na Madereva watatu walipewa fedha Kwa ajili ya kununua Mabati hayo lakini badae iliripotiwa kuwa  Mabati yameibiwa Huku milango wa stoo ikiwa haijavunjwa.

 Kwa sasa watuhumiwa Wote wanashikiliwa na jeshi la polisi na upelelezi utakapo kamilika watafikishwa mahakamani.

KWA TAARIFA ZAIDI TAZAMA VIDEO HII