Wabunge Josephat Gwajima (Kawe) na Jerry Silaa(Ukonga) ambao ni wajumbe wa kamati ya kudumu ya bunge ya Haki,Kinga na Mamlaka ya Bunge wameondolewa kwenye kamati hiyo hadi itakapoamuliwa vinginevyo.
Kamati ambayo wameondolewa wabunge hao ndiyo inayowahoji kuhusu tuhuma mbalimbali zinazowakabili.
Mnamo agosti 21 mwaka huu Gwajima na Silaa waliitwa mbele ya kamati ya Maadili ya Bunge kujibu tuhuma zinazowakabili ikiwemo ya kusema uongo na kushusha hadhi na heshimaya Bunge
0 Comments