Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru 2021 Luteni Josephine Mwambashi amewataka wananchi wa Lindi kutunza na kulinda miundombinu ya vyanzo vya maji ili huduma hiyo iwe endelevu.

Hayo ameyasema wakati akikagua miradi mbalimbali mkoani humo huku akiwataka watendaji kuwapa wananchi taarifa za miradi hiyo kwani ni haki yao kuifahamu.