Mbunge wa jimbo la Ukonga Jerry Silaa leo ameeleza sababu ya kushindwa kufika katika kikao hapo jana kwa ajili ya kuendelea kuhojiwa na kamati ya Kudumu ya Bunge haki, maadili na madaraka ya bunge kwamba hakuwa na taarifa na pia alikuwa na matatizo ya kiafya.

Akizungumzia suala hilo Mwenyekiti wa kamati ya Kudumu ya Bunge haki, maadili na madaraka ya bunge Emmanuel Mwakasaka amesema leo wamekamilisha shauri lake la mahojiano na kwamba suala la yeye kutokufika kikaoni hapo jana kutokana na sababu zake kamati inalifanyia kazi.