AJALI YA BODABODA YAUA PAPO HAPO WATATU



WATU watatu wakazi wa Ngofila wilayani Kishapu mkoani Shinyanga, wamefariki dunia Papo hapo, baada ya kugongwa na gari  wakiwa wamebebana mshikaki kwenye bodaboda.

Akitoa taarifa hiyo kwa vyombo vya habari,  Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani Shinyanga George Kyando,  amesema ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 1 asubuhi katika barabara ya Ngofila- Igulumbi Kata ya Ngofila wilayani Kishapu.

Kyando amewataja watu hao kuwa ni Konya Jiloma ambaye ni dereva wa bodaboda, Mipawa Njile na Ndosera Maganga ambao ni abiria waliokuwa wamebebwa mshikaki, ambapo waligongwa na gari aina ya Scania Lori lenye namba za usajili T.550 AJA, na kusababisha vifo vyao papo hapo.


“Chanzo cha Ajali hii ni mwendokasi wa dereva wa pikipiki, ambapo alilivamia gari hilo na kusababisha ajali ambayo imepelekea vifo vyao,”Kyando.

Ameongeza kuwa Jeshi linamtafuta dereva wa gari hilo Salimu Abdalla, ambaye alikimbia kusikojulikana mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo.

Aidha Kamanda ametoa wito kwa madereva wa vyombo vya moto kuzingatia sheria za usalama barabarani, na kuacha kuendesha kwa mwendokasi, na kusababisha ajali za uzembe ambazo zina gharimu maisha ya watu.

Post a Comment

0 Comments