Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Anthony Lugendo, miaka 34, mkulima mkazi wa Mlandizi kwa kosa la kumdhalilisha mtoto mdogo wa kike miaka 3, (Jina limehifadhiwa) kwa kumchezea sehemu za siri.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kibaha mkoani Pwani Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani ACP Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo mnamo tarehe 16/9/2021 majira ya saa 10 jioni huko kitongoji cha Kaloleni, kata ya Janga, Wilaya ya Mlandizi mkoa wa Pwani.
Kamanda Nyigesa amesema mtuhumiwa alikamatwa akiwa chumbani kwake amemvua nguo na akiwa anamchezea chezea sehemu za siri mtoto huyo ambaye ni mwanafunzi wa Chekechea.
0 Comments