Jeshi la Polisi linamshikilia mwanamke aitwaye Fatuma Juma Charles (22), mhudumu wa bar kwa uchunguzi kwa tuhuma za kusababisha kifo cha Mlinzi wa Kampuni ya Ulinzi ya Mast Holding aitwaye Steven Felician Samandari (25) ambaye ameuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa Bar/Guest kwa ajili ya mapenzi Mjini Kahama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando akitoa taarifa kwa vyombo vya habari, amesema tukio hilo limetokea Septemba 11,2021 majira ya saa nane usiku katika mtaa wa Nyahanga kata ya Nyahanga Manispaa ya Kahama.
“Chanzo cha tukio hilo ni kufuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi. Eneo la tukio kimeokotwa kisu kikiwa tumboni. mbinu iliyotumika ni kuchoma kisu tumboni. Mlinzi huyo aliuawa kwa kuchomwa kisu tumboni na mtu aliyekuwa amemkamata baada ya kuruka uzio akifuatilia wahudumu wa bar/guest kwa ajili ya mapenzi,” amesema Kamanda Kyando.
0 Comments