Mashabiki na wapenzi  wa klabu ya Simba wamefurika katika Uwanja wa Mo Simba Arena kwa ajili ya kushiriki dua maalum ya kumuombea aliyekuwa Mjumbe wa Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji TFF na Kiongozi wa Simba Sc, ndugu, Zacharia Hans Pope.

Hans Poppe amefariki dunia Ijumaa Septemba 10 wakati akipatiwa matibabu katika hospitali ya Aga Khan Dar es Salaam.