Baada ya Yanga kuruhusu kipigo cha bao 1-0 dhidi ya Rivers United ya Nigeria kwenye uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema wanajipanga kwa ajili ya mechi ya marudiano Septemba 19 nchini Nigeria na kwamba hawakuwa na maandalizi mazuri.
"Leo tumepoteza mechi ya nyumbani, tunakiri maandalizi yetu ya pre season hayakuwa mazuri, ni kama hayakuepo ila tunajipanga," amesema Mwakalebela.
0 Comments