Bruno Fernandes 

Manchester United wamekuwa na mazungumzo mazuri na kiungo wa kati wa Ureno Bruno Fernandes tangu mwezi Julai. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 anataka kusalia Old Trafford na kandarasi yake inachukuliwa na umuhimu mkubwa pamoja na kiungo wa kati Paul Pogba, 28.

Kalidou Koulibaly,

United ilitaka kufanya mazungumzo ya makubaliano na Napoli ili kumsajili nahodha wa Senegal Kalidou Koulibaly, 30, msimu ujao lakini hawakuwa tayari kukubali thamani ya mchezaji huyo kama inavyodaiwa na klabu hiyo ya Serie A ya £34m kumnunua beki huyo wa kati.Source:BBC