Mwanamke mmoja  mkazi wa Bushushu Mjini Shinyanga  amenusurika kifo baada kushambuliwa kwa kupigwa sehemu mbalimbali za mwili wake kisha kukatwa mkono wa kushoto kwa kisu na mme wake kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mwanamke huyo aliyejulikana kwa jina la Debora Rwekwama (34) ambaye ni Mfanyakazi wa Benki ya CRDB ameshambuliwa na mume wake aitwaye Jacobo Mwajenga (35) .

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP George Kyando amesema tukio hilo limetokea Septemba 9,2021 usiku katika mtaa wa Bushushu, Manispaa ya Shinyanga.

Ameeleza kuwa hali ya majeruhi ni mbaya na amelazwa katika hospitali ya wilaya Kahama.

Amesema chanzo cha tukio ni wivu wa mapenzi na kwamba tayari Jeshi la Polisi linamshikilia mtuhumiwa wa tukio hilo.