
Watu wawili ambao ni wapenzi wamekutwa wamefariki katika makazi yao kwa kunywa sumu katika kitongoji cha Mlandizi kata ya landizi tarafa ya Mlandizi wilaya ya kipolisi Mlandizi huko mkoani Pwani.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Pwani Wankyo Nyigesa amesema tukio hilo limetokea mnamo septemba 5 ,2021 majira ya asubuhi chanzo kikidaiwa kuwa ni wivu wa kimapenzi ambapo mwanaume alitengeneza juisi ambayo ndani yake ilikuwa na sumu na kumpa Veronica akanywa na kufariki ,na baada ya kuona mpenzi wake amefariki nae akanywa akafariki.
"Chanzo ni wivu wa kimapenzi ambapo mwanaume alikuwa akimtuhumu Veronica kuwa anafanya usaliti ,kwenye eneo la tukio tumekuta chupa yenye masalia ya sumu na pia tumekuta karatasi inayodhaniwa kuandikwa na mmoja wao na imeandikwa ' Huu ni Usaliti tu',". Kamanda Nyigesa
Amewataja wapenzi hao kuwa ni Godfrey Pius Mandai (48) dereva na Veronica Gerald(42) mkazi wa Mtwara ambaye alikuja Mlandizi kumfuata mpenzi wake.
0 Comments